• Home

SwahilizoneTz

  • Mwanzo
  • Tanzania
  • Afrika Mashariki
  • Kimataifa
    • Bara
      • Afrika
      • Anwani zetu
      • Asia
      • Ulaya
      • Ocenia
    • Ulinzi na Amani
    • Maendeleo
    • Afya
  • Takwimu
  • Matukio
  • michezo
  • sheria
  • Makala
  • Zaidi
    • Ripoti Maalum
    • City FM Radio
    • Picha
    • Washirika
  • Afya
Showing posts with label Tanzania. Show all posts
Kijana Novat Carol Ambae alimaliza chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na kukosa Kazi na kujikuta akianzisha kituo cha Kijamii Wilayani Sengerema MKoani Mwanza Elimu living Labaratory

Wawakilishi wa mataifa matatu ya bara Asia walipokutana mapema leo
Hatimaye Malaysia, Thailand na Indonesia zimekubaliana kuwapa makazi ya muda wahamiaji elfu saba waliokwama kwa siku kadhaa kwenye pwani ya mataifa hayo.
Hayo yameafikiwa na mawaziri wa mashauri ya kigeni wa mataifa hayo katika mkutano uliokuwa ukiendelea mjini Kuala Lumpur.
Mawaziri hao wamesema kuwa hatua hiyo ya muda ya kuwapa usaidizi wakimbizi hao,wanaotoka kwa kabila dogo la waislamu wa Rohingya kutoka Mynmar na Bangladesh,
Wahamiaji waliokwama baharini Waokolewa
kutaipa muda jamii ya kimataifa kuwatafutia sehemu ya kudumu, katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Mataifa hayo matatu ya Malaysia, Indonesia na Thailand, yamekosolewa sana kwa kukataa kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia katika mataifa yao.
Mynmar ilikataa kuhudhuria mkutano huo na badala yake ikaandika barua ikielezea namna ya itakavyokabiliana na swala hilo la uhamiaji.
Msemaji wa shirikisho linalosimamia maswala ya wahamiaji ILO Jeff Labovitz ameiambia BBC kuwa hatua hii ya dharura itasaidia sana kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi ambao wamekuwa wakihangaika baharini bila chakula wala muundo msingi wa afya.
Wavuvi nchini Indonesia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano
Bado kuna hofu kuhusu usalama na afya ya wale waliokwama baharini ambao wanahitaji chakula na maji.
Wavuvi nchini Indonesia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano
Maelfu ya raia kutoka Bangladesh na Waislamu jamii ya Rohingya wamekuwa katika bahari ya Andaman kwa majuma kadhaa sasa baada ya serikali ya Indonesia kubadili sheria ilikukabiliana na walanguzi wa watu kupitia bahari na ardhi yake.
Thailand,Malaysia na Indonesia zilikuwa zimekataa kuwaruhusu wamahiaji kuingia katika pwani za nchi zao
Huku hayo yakijiri, mashua moja iliyokuwa imewabeba wahamiaji mia nne, na ambayo ilikuwa imenyimwa ruhusa ya kutia nanga katika mataifa matatu ya bara Asia, sasa imewasili katika kisiwa cha Aceh, nchini Indonesia.
Mashua hiyo imekuwa baharini kwa miezi miwili unusu ikiwa imewabeba wahamiaji wa kiislamu wa kabila la Rohingya kutoka nchini Myanmar.
Mashua hiyo iliyopigwa picha na BBC juma lililopita ilipokuwa imekwama katika maji ya mipaka ya Thailand, ilikuwa na tatizo la Injini.

Chanzo bbc

Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi
Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu zilizofuatia ni bora kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.
''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Mei lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.'' alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
''Subiri tu'' Nyamitwe aliwaambia waandishi wa habari.
Wanajeshi waaminifu kwa Nkurunziza walizima jaribio la mapinduzi juma lililopita
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba amesema kuwa tayari rais Nkurunziza ametia sahihi amri hiyo ya kuhairishwa kwa uchaguzi.
Umoja wa mataifa ya bara Ulaya EU, na Umoja wa mataifa ya Afrika AU, yametoa wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata mkubwa uhairishwe ilikutoa fursa kwa mazungumzo ya upatanishi kuendelea .
Hapo jana Rais wa Afrika Kusini alitilia pondo hoja hiyo ya kuahirisha uchaguzi akisema ni bora uchaguzi huo uliopangwa ''uhairishwe''.
Takriban watu 20 wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na waandamani katika mji mkuu wa Bujumbura kilele ikiwa ni juma lililopita makamanda waasi walipotangaza jaribio la mapinduzi rais
Nkurunziza akiwa mjini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda uliolenga kutatua mzozo wa kisiasa nchini mwake.
Waandamanaji wamekuwa wakipinga kauli ya Nkurunziza ya kutaka kuwania muhula wa tatu
Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangazwa kwake nia ya kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani ya mwaka wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 13.
Nkurunzizakwa upande wake anashikilia kukutu kuwa ana haki ya kuwania muhula mwengine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na wanainchi bali wabunge.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Chanzo:BBC
    
   
Real madrid washangazwa na Valencia baada ya kutoka sare 2-2

Kilabu ya Real Madrid iligonga mwamba wa goli mara tatu huku nyota wake Christiano Ronaldo akikosa penalti na hivyobasi kupata sare ya 2-2 na timu ya Valencia hatua iliodidimiza matumaini yao kubeba taji la ligi hiyo.
Real ilitoka nyuma 2-0 na kupata sare hiyo na hivyobasi kuweka pengo la pointi nne kati yao na viongozi wa sasa Barcelona huku ikiwa imesalia mechi mbili.
Paco Alcacer aliipatia Valencia ilio nafasi ya nne katika jedwali uongozi kabla ya Javi Fuego kufunga la pili.
Mkwaju wa penalti uliopigwa na Ronaldo uliokolewa kabla ya Pepe kufunga bao la kwanza na Isco kuongeza bao la kusawazisha.Real Madrid pia ilipata pigo jingine baada ya kumpoteza Tony Kroos na jeraha katikati ya kipindi cha kwanza.

                           




 
Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza akiwasilisha stakhabadhi zake za kutaka kuwania urais kwa muhula wa tatu

Wapinzani wa raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza wamepuuza agizo la serikali la kuwataka wasitishe maandamano ya wiki mbili wakilitaja agizo hilo kuwa sawa na kutangaza vita.
Hadi sasa watu 18 wameuawa tangu rais Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula wa tatu kwenye uchaguzi wa mwezi ujao.
Waandamanaji wachoma matairi katika vizuizi vya barabarani kupinga hatua ya Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu
Katika maeneo mengine waandamanaji waliweka vizuizi katika barabara usiku kucha kinyume na agizo la serikali ambalo lilitolewa siku ya jumamosi kwamba vizuizi vyote viondolewe katika kipindi cha saa 48.
Habari zinazotufikia zinasema kuwa watu wawili zaidi wamedaiwa kuuawa katika maandamano hayo na kuongeza idadi ya waliouwa kufikia 20.

Mshirikishe mwenzako     

  • Facebook
  • Twitter
  • WhatsApp
Shughuli za kutafuta manusura Nepal.

Matumaini yanadidimia nchini Napal ya kuwapata manusura zaidi baada ya kutokea kwa tetemeko baya la ardhi wiki moja iliyopita .
Msemaji wa wizara ya ndani ya nchi hiyo (Laxmi Prasad Dhakal) alisema, anafikiri kuwa hakuna uwezekano wa kupata manusura zaidi waliofukiwa chini ya vifusi.
Alisema kuwa idadi ya waliokufa sasa imezidi watu 6,600. Maelfu ya watu bado hawajulikani waliko wakiwemo raia zaidi ya 1000 kutoka nchi za ulaya.
Takriban helkopta ishirini zinashiriki katika jitihada za uokoaji katika vijiji vya mbali maeno yaliyo kaskazini mwa nchi.
CHANZO BBC
helikopta
Mamlaka ya Nepal imeomba msaada zaidi wa helikopta kutoka kwa mataifa ya kigeni baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko baya la ardhi ambapo zaidi ya watu elfu sita waliuawa.
Serikali imesema inahitaji ndege hizo kusafirisha misaada ya dharura katika maeneo ya vijiji hususan maeneo ya milimani.
Nepal tetemeko
Pia ndege hizo zitasaidia kuwasafirisha majeruhi ili kupokea matibabu.
Kumekua na makabiliano miongoni mwa manusura wanaong'angania usafiri mdogo ambao unatolewa na serikali.
Nepal
Serikali pia imetaka maiti zote kuzikwa punde baada ya kutolewa ndani ya vivusi.
Waziri wa fedha wa Nepal , Ram Sharan Mahat, amesema nchi yake inahitaji dola bilioni mbili kukarabati nchi hiyo ambayo miundo msingi yake imeharibiwa vibaya.

Mwanadada Mrembo kutoka Rock city mwanza Susan sechuma A.K.A suziety ameibuka na kusema Mrembo wa Kiganda Zari Hassan  a.k.a Rarithe boss lady kuwa anawafanya watanzania kuwasahau mastar wao . Susy Anasema kitendo cha vyombo vya Habari kuremba kila mara kwenye Tv na radio sio sawa, Anasema kila mara ni habari za zari na Diamomd ndo kusema Wema au wolper hawana kipya , susan sechuma anasema Hii inatufanya tuweze kuwasahau mastar wetu kama vile wema,
Suz aliwai kuwa mwigizaji na alifanya kazi kadhaa kabla ya kuamua kujiunga na chuo kikuu cha Sauti cha jiji mwanza. Na kwa sasa yupo anafanya kazi zake binafsi huko jijini mwanza

Alie wai kuwa waziri wa Nishati na Madini Mh Wiliam Ngeleja amesema Pesa za Escrow Hazikuwa pesa za  umma bali zililuwa pesa za Mtu binafsi Na aliomba msaada kama mtu mwingine vile amabvyo anaweza kuomba pesa anasema Ni kweli alipokea kiasi cha shilingi millioni arobain na laki Nne na anasema alilipa kodi millioni kumi na tatu na serkali ilipokea katika ufafnuzi wake anasema tangu lini mwizi analipa kodi kwa mamlaka na anakuwa huru akiulizwa swali na mtangazji Bwana Alloyce Nyanda Kuwa ilikuaje mpaka ukahojiwa na kamati ya Maadili kama hukuchukua pesa na Tangu lini mtu asiemwizi anaweza kuhojiwa na Kamati kulitokea nini katika kulijibu hilo Mh ngeleja alisema ni utaratibu tu wa kawaida tu mtu anaetuhumiwa kuhojiwa lakin hujasikia Kamati imesema mimi mwizi wala mahakama haijasema na Navyojua mtu mwizi huwa yupp tumande au mahakamn lakin mimi nadunda na nipo hapa katika interview yalikuwa majibu ya mh ngeleja
Waandamanaji wakipinga vifo vya wahamiaji wanaovuka bahari ya shamu kwenda Ulaya
Makundi ya kupigania haki za kibinadamu yamesema kuwa mikakati ilioafikiwa na muungano wa ulaya kuzuia idadi kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka hadi Ulaya kutoka Afrika sio ufumbuzi wa tatizo hilo
.
Katika kikao cha dharura kilichofanyika mjini Brussels siku ya alhamisi, Viongozi wa Ulaya walikubaliana kuongeza msaada wao mara tatu ili kuimarisha usakaji na uokozi wa wahamiaji katika bahari ya shamu.
Pia waliidhinisha mikakati ya kukamata na kuharibu vyombo vinavyotumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao.
Lakini Shirika la Human Rights Watch pamoja na lile la kuwasaidia watoto la Save the Children, yanasema kuwa EU inafaa kuongeza juhudi zake katika uokoaji badala ya kullinda mipaka yake.
Mkutano huo uliitishwa baada ya zaidi ya watu 800 kuuawa wikendi iliopita baada ya boti yao kuzama.

Mshirikishe mwenz

Waafrika Kusini waandamana kupinga xenophobia
Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini wameandamana katika mji mkuu wa kibiashara wa nchi hiyo, Johannesburg
Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo
Na Bakari Kimwanga, Mwanza
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe
Polisi nchini Somalia wanasema kuwa takriban watu Saba wameuawa kwenye shambulizi lililolenga gari la Umoja wa Mataifa katika eno linalojisimamia la Puntland
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuungana kwa pamoja katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama nchini Ethiopia, Rais uhuru Kenyata
Mtangazaji maarufu wa kituo cha habari na mawasailiano cha sengerema Telecentre Kupitia radio ya sengerema 98.8 kilichoko wilaya ya semgerema mkoani mwaza DUAH JULIUS amezungum,na swahilizonetz na kufunguka kuhusu jinsi ndoto yake ya kusakata kabumbu katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ilivyoweza kuzima na kujikuta akiwa mtanagazji wa michezo.
Duah julius(Mtangazji radio sengerema)

Shughuli za upigaji kura zinaendelea nchini Liberia kuwachagua maseneta wapya licha ya kuwepo kwa hofu kwamba kura hiyo huenda ikachangia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Kundi la waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kukiuka sheria ya msamaha kwa waasi wa kundi hilo.
Taarifa iliyotolewa na Tawi la Kisiasa la kundi la M23 imesisitiza kwamba serikali ya Kongo kabla ya kutangaza msamaha, ilitoa orodha ya majina ya mamia ya wanachama wa kundi hilo akiwemo Jenerali Sultani Makenga na baadhi ya makamanda wengine wa kundi hiyo, na kueleza kwamba watu hao hawana sifa za kupewa msamaha. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua ya kutayarishwa orodha hiyo inakinzana waziwazi na taarifa ya pamoja iliyotolewa Nairobi, Kenya  pamoja na msamaha waliopewa waasi wa kundi hilo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Februari mwaka huu, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alitangaza msamaha kwa waasi wote wa kundi la M23, isipokuwa wale waliotenda jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu.
Shuhuda wa ajali hiyo, Paulina Ruge (57) ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyogongwa na basi hilo, alisema ilitokea kati ya saa 4:30 na 5:00 asubuhi.

BUSEGA.
 

Watu 10 wamekufa papo hapo na mwingine kupoteza maisha alipokuwa akipelekwa hospitali baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali mkoani Simiyu.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Itwilima A, Kata ya Kilorei, Wilaya ya Busega baada ya basi hilo la Luheye lifanyalo safari zake kati ya Bunda na Mwanza kupata hitilafu na kugonga mti na baadaye nyumba.


Akizungumza katika Hospitali ya Wilaya ya Magu jana, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Pascal Mabiti alisema watu waliokufa ni 11 na majeruhi 44.


Mabiti alisema mtu mmoja aliyefariki wakati akipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jina lake bado lina utata... “Jina la huyu mama ambaye ameacha watoto watatu; Joyce Wilson (6), Jenipher Wilson (3) na Jack (miezi miwili), wametwambia mama yao alikuwa anaitwa Lucia Wilson, lakini taarifa tulizopata kutoka Bugando zinasema alikuwa anaitwa Fodia Guniniga.”


Alisema majeruhi 19 ni wanawake na 25 wanaume na kwamba, wachache wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu lakini wengi walipelekwa Bugando kutokana na hali zao kuwa mbaya. “Natoa wito kwa wananchi kwenda Hospitali ya Bugando Mwanza kutambua maiti. Miili ya watu wote waliokufa tumeihifadhi hapo na hakuna aliyetambuliwa zaidi ya huyo mama ambaye ameacha watoto watatu,” alisema.


Shuhuda wa ajali hiyo, Paulina Ruge (57) ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyogongwa na basi hilo, alisema ilitokea kati ya saa 4:30 na 5:00 asubuhi.


Alisema baada ya ajali alishuhudia ikitolewa miili ya watu 10 waliokufa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema baada ya kutokea ajali hiyo dereva ambaye jina lake halijafahamika alikimbia na polisi wanaendelea kumtafuta.MWANANCHI
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.

Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirin
Older Posts Home

Habari za Ulimwengu (audio)

Matangazo ya Radio

Matangazo ya Radio
Aloyce Nyanda

Kutoka Bungeni

Waliokwisha Peruzi

swahilizonetz

swahilizonetz

Habari kwa Kina

Habari kwa Kina

Habari

Afrika afrika mashariki Amani na Ulinzi Asia Makala michezo Siasa Tanzania Uchumi na Biashara Ushirikiano Kimataifa
swahilizonetz. Haki zote zimehifadhiwa.
Imeendelezwa na swahilizonetz