• Home

SwahilizoneTz

  • Mwanzo
  • Tanzania
  • Afrika Mashariki
  • Kimataifa
    • Bara
      • Afrika
      • Anwani zetu
      • Asia
      • Ulaya
      • Ocenia
    • Ulinzi na Amani
    • Maendeleo
    • Afya
  • Takwimu
  • Matukio
  • michezo
  • sheria
  • Makala
  • Zaidi
    • Ripoti Maalum
    • City FM Radio
    • Picha
    • Washirika
  • Afya
Showing posts with label Ushirikiano Kimataifa. Show all posts
Shughuli za kutafuta manusura Nepal.

Matumaini yanadidimia nchini Napal ya kuwapata manusura zaidi baada ya kutokea kwa tetemeko baya la ardhi wiki moja iliyopita .
Msemaji wa wizara ya ndani ya nchi hiyo (Laxmi Prasad Dhakal) alisema, anafikiri kuwa hakuna uwezekano wa kupata manusura zaidi waliofukiwa chini ya vifusi.
Alisema kuwa idadi ya waliokufa sasa imezidi watu 6,600. Maelfu ya watu bado hawajulikani waliko wakiwemo raia zaidi ya 1000 kutoka nchi za ulaya.
Takriban helkopta ishirini zinashiriki katika jitihada za uokoaji katika vijiji vya mbali maeno yaliyo kaskazini mwa nchi.
CHANZO BBC
Polisi nchini Somalia wanasema kuwa takriban watu Saba wameuawa kwenye shambulizi lililolenga gari la Umoja wa Mataifa katika eno linalojisimamia la Puntland
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuungana kwa pamoja katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama nchini Ethiopia, Rais uhuru Kenyata
Shuhuda wa ajali hiyo, Paulina Ruge (57) ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyogongwa na basi hilo, alisema ilitokea kati ya saa 4:30 na 5:00 asubuhi.

BUSEGA.
 

Watu 10 wamekufa papo hapo na mwingine kupoteza maisha alipokuwa akipelekwa hospitali baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali mkoani Simiyu.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Itwilima A, Kata ya Kilorei, Wilaya ya Busega baada ya basi hilo la Luheye lifanyalo safari zake kati ya Bunda na Mwanza kupata hitilafu na kugonga mti na baadaye nyumba.


Akizungumza katika Hospitali ya Wilaya ya Magu jana, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Pascal Mabiti alisema watu waliokufa ni 11 na majeruhi 44.


Mabiti alisema mtu mmoja aliyefariki wakati akipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jina lake bado lina utata... “Jina la huyu mama ambaye ameacha watoto watatu; Joyce Wilson (6), Jenipher Wilson (3) na Jack (miezi miwili), wametwambia mama yao alikuwa anaitwa Lucia Wilson, lakini taarifa tulizopata kutoka Bugando zinasema alikuwa anaitwa Fodia Guniniga.”


Alisema majeruhi 19 ni wanawake na 25 wanaume na kwamba, wachache wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu lakini wengi walipelekwa Bugando kutokana na hali zao kuwa mbaya. “Natoa wito kwa wananchi kwenda Hospitali ya Bugando Mwanza kutambua maiti. Miili ya watu wote waliokufa tumeihifadhi hapo na hakuna aliyetambuliwa zaidi ya huyo mama ambaye ameacha watoto watatu,” alisema.


Shuhuda wa ajali hiyo, Paulina Ruge (57) ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyogongwa na basi hilo, alisema ilitokea kati ya saa 4:30 na 5:00 asubuhi.


Alisema baada ya ajali alishuhudia ikitolewa miili ya watu 10 waliokufa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema baada ya kutokea ajali hiyo dereva ambaye jina lake halijafahamika alikimbia na polisi wanaendelea kumtafuta.MWANANCHI
Uchunguzi wa kina wa Swahilizone umethibitisha kuwa baadhi ya wakazi wa mpaka wa Niger na Nigeria wamekuwa wakishirikiana na wapiganaji wa Boko Haram ili walipwe pesa.
Nchi zilizo jirani na Nigeria, kama Niger, Cameroon, na Chad zinahofia kuwa harakati za wanamgambo hao zitaathiri usalama wa nchi hizo.
Kulingana na Thomas Fessy ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi huo akiwa eneo la Diffa kusini mashariki mwa Niger katika mpaka na Nigeria, wanachama wa genge hilo ambao wengi wao ni vijana walio na umri wa miaka kati ya 20 na 25 wameiambia BBC kuuwa vikundi vyao vitano vimeshajiunga na Boko Haram; na wawili tayari walishauawa katika operation walizojihusisha nazo.
Mpaka kati ya Niger na Nigeria.
Wanadai Boko Haram waliwapa dollar 3,000 ndio wajiunge nao.
Lakini wamesisitiza wao hawana haja na kupigania uwepo wa sheria za kiislamu , haja yao ni hizo pesa.
Maafisa wa usalama katika eneo hilo wanasema wamemudu kuzuia mashambulio kadhaa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita na watu kadhaa wanaoaminika kuwa na uhusiano na Boko Haram wamekamatwa.
Ni dhahiri kuwa Boko Haram wanaendeleza vitendo vyao vya kikatili hadi kuvuka mpaka wa Nigeria.
Umoja wa mataifa unasema tayari watu wapatao 50,000 washavuka mpaka kuingia Niger kujaribu.
Kumekuwa na Malumbano baina ya Ukraine na Urusi katika Umoja wa Mataifa huku kila upande ukimshutumu mwenzake kuwa gaidi
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma kikosi kipya cha wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-kikosi hicho kitawajumuisha wanajeshi karibu alfu kumi na mbili.
Marekani imelaani kile imekitaja kuwa hatua ya Urusi kutumia kaiwi kama chombo cha kuishurutisha Ukraine.
Madaktari wa idara ya afya ya akili mkoani mwanza jana wameazimisha siku ya kifafa duniani
inayoadhimishwa tarehe 26 march kila mwaka duniani kote.Akizungumza na wanahabari daktari mkuu wa idara ya afya ya akili katika hosptari ya rufaa ya BUGANDO(BMC)
Matukio ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China kwa kesi za biashara ya dawa za kulevya yana idadi kubwa sana ndani ya hii miaka mitano iliyopita

Jeshi la Polisi Nchini litaendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na vitendo vya mauaji yanayosababishwa na Imani za kishirikina kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IJP Ernest Mangu katika mkutano mkuu wa maofisa wakuu waandamizi unaoendelea katika chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA) ukiwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Weledi katika Kutoa Huduma bora kwa jamii”.
JP Mangu alisema kuna baadhi ya jamii zinafanya vitendo hivyo kama tamaduni zao hivyo wao kwa kuliona hilo wataendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ili kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa hapa nchini.
“Tuendelee kutoa elimu kwa jamii lakini pia tutaenelea kuchukua hatua kwa wote wanaofanya makosa hayo kwa kuwa huo ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine” Alisema IJP Mangu.
Naye Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amewataka Makamanda wa Polisi wa mikoa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali katika kutatua migogoro ya Ardhi ili kuipatia ufumbuzi mapema kabla ya vurugu kutokea jambo ambalo litaendeleza usalama hapa nchini.
Alisema ni vyema Taasisi husika kushirikiana mapema katika kutatua migogoro katika jamii kabla haijaleta madhara kwa kuwa iwapo hilo litafanyika itaepusha uharibifu na gharama ambazo hutumika katika kutatua mgogoro unapokuwa mkubwa na kusababisha vurugu.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Jamii nchini Mussa Ali Mussa alisema wataendelea kutumia dhana ya Polisi Jamii katika kupambana na uhalifu kabla haujatokea kwa kuwa wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa tangu kuanzishwa kwa dhana hiyo.
Alisema kwa Mujibu wa Utafiti uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ufadhili wa COSTEC umeonyesha kuwa Asilimia 70 ya watanzania wamekubali dhana ya Polisi Jamii na wameonyesha kuikubali kwa kuwa imesaidia kupambana na uhalifu unaotokea katika maeneo yao.
Mkutano huo unaoendelea katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi una lengo la kujadili na kufanya tathmini ya mafanikio yaliyofikiwa mwaka 2013 pamoja na changamoto zilizopo katika kupambana na uhalifu na kuzipatia ufumbuzi kwa mwaka 2014.
ESHI la Polisi Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya limemtia mbaroni askari wa Kikosi cha KMKM, Hussein Soud Hussein (30) baada ya kukamatwa na dawa za kulevya jumla ya kete 270 katika eneo la Darajabovu mjini Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Upelelezi na Makosa ya Jinai Yussuf Ilembo alithibitisha kukamatwa kwa askari huyo na kusema inasikitisha sana kuona askari ambaye ndio tegemeo la kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya anajishughulisha na biashara hiyo haramu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa

“Ni kweli tumemkamata kijana mmoja Hussein Soud Hussein ambaye baada ya kumfanyia usaili alikiri na kuthibitisha kwamba yeye ni askari wa Kikosi cha KMKM na tuliona kitambulisho chake,” alisema Ilembo.
Ilembo alisema askari huyo alikamatwa ikiwa sehemu ya msako unaoendelea wa Jeshi la Polisi pamoja na Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya kuwatafuta wauzaji na wasambazaji wa dawa hizo.
Kukamatwa kwa askari huyo kunatokana na taarifa kutoka kwa raia wema ambao walichukizwa na tabia yake ya kufanya biashara ya dawa za kulevya wakati akiwa askari wa ulinzi.
Alisema kwa sasa Polisi wapo katika doria endelevu ya kuwatafuta vijana wanaofanya biashara ya dawa za kulevya katika maeneo ya mjini na vijijini.
Taarifa zaidi ziliopo sasa kwa mujibu wa Jeshi la Polisi ni kwamba biashara ya dawa za kulevya hufanywa zaidi vijijini kutokana na msako wa Polisi Jamii ulioshamiri mjini ambao hautoi nafasi kwa wafanyabiashara hao kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Chanzo: Habari Leo
WANAWAKE DAY


KAULI MBIU YA MWAKA 2014




CHOCHOEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA


Afisa Jinsia wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita madawa ya kulevya (OJADACT) Shani Saidi Amanzi amewataka wanawake siku hiyo iwe ni siku pekee ya kuonyesha uelewa wao mjini tu bali waweze kuwakumbuka na wanawake walio vijijini .
Shani amesema wanawake wengi kwa sasa wanaupeo mkubwa wa mambo mbalimbali na wanajitambua mfano mzuri ni bunge la katiba pia usawa wa wanawake na wanaume umetendeka kuwepo bungeni.
Aidha sakata kubwa linalowapa doa wanawake kwa sasa ni matumizi ya madawa ya kulevya ambapo kwa tamaduni za kiafrika tendo hilo ni tendo lenye muonekano kwa mwanamke kuonekana kama mtu mwenye roho ngumu na mwiko kwa mwanamke .
Akiwa kama Afisa Jinsia anayehusika na maswala ya kijinsia hasa watoto na wanawake anasikitishwa sana kuona jamii imebadilika hususani aibu ya mwanamke  haionekani hasa kwenye kufanya maovu  .
Mfano mzuri sakata la kutumika kwa madawa ya kulevya  kwa sasa ni kama  biashara  na matumizi mfano mzuri ni sakata la wanawake wengi maarufu kutumia madawa ya kulevya mfano mzuri ni Masogange na Melisa kukamatwa kule Afrika Kusini na
Jack Patrick ambaye alikamatwa Hongkong china Decemba 19 mwaka 2013 ambaye pia ni mwanamitindo na alikuwa  Miss Ilala Namba 3, 2005, alikamatwa na madawa aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 kwa kuhifadhiwa ndani ya kete 57.

Shani amewataka wanawake na wasichina wanaotumia madawa ya kulevya kutokana na sababu mbalimbali waache kabisa  na kujihusisha na shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo.
Shani amesema kwa kushirikiana na waandishi wa habari atahakikisha mambo ya kijamii hasa kwa watoto na kina mama yanakuwa katika mstari wa mbele katika kuyaandika ,kuyaonyesha na wanajamii kuyasikia  yawe mabaya au mazuri ili kukosoa,kuelimisha  na kukemea ili kuleta maendeleo ndani ya nchi.
Kwani kauli mbiu ya kitaifa  mwaka  huu inasema chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia ambapo kwa mkoa wa Mwanza maandamano yataanza kuanzia Nyakato sokoni paka shule ya msingi Nyakato kata ya Mahina.





Thailand does have the death penalty for various offences. Here are examples of crimes which may get a convicted offender sentenced to execution by the state.

Death Penalty Statistics : 25th February 2014

Total number of prisoners condemned to death 685 persons
Male                       630 persons
Female                     55 persons
 

Total                       685 persons

Antiretroviral resistance could increase if untreated HIV-infected individuals exposed to antiretroviral medication

August 28, 2013 — A new study led by researchers at Harvard School of Public Health (HSPH) calls attention to a new street drug being used in South Africa. Known as whoonga, the drug cocktail may combine HIV antiretroviral (ARV) medication with illicit drugs. Believed to be extremely addictive, whoonga appears to have a devastating impact on those who use it—including children—and has the potential to complicate efforts to combat the HIV epidemic
Utumiaji wa madawa ya kulevya ni mojawapo ya mabalaa makubwa yanayoathiri binaadamu na ulimwengu kijumla.  Watu wengi wameathiriwa na janga hili biladi/miji zetu
Moshi.Raia watatu wa kigeni waliokamatwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA), wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kusomewa mashtaka matatu tofauti
illustration of a neuron
Drugs of abuse alter the way people think, feel, and behave by disrupting neurotransmission, the process of communication between brain cells. Over the past few decades, studies have established that drug dependence and addiction are features of an organic brain disease caused by drugs' cumulative impacts on neurotransmission. Scientists continue to build on this essential understanding with experiments to further elucidate the physiological bases for drug abuse vulnerability as well as the full dimensions and progression of the disease. The findings provide powerful leads to new medications and behavioral treatments.
This second article in our NIDA Notes Reference Series discusses the central importance of studying drugs' effects on neurotransmission and describes some of the most common experimental methods used in this research. As with other articles in the series, we provide illustrative references from articles published in NIDA Notes.

What is Neurotransmission?

A person reads. The words on the page enter the brain through the eyes and are transformed into information that is relayed, from cell to cell, to regions that process visual input and attach meaning and memory. When inside cells, the information takes the form of an electrical signal. To cross the tiny intercellular gap that separates one cell from the next, the information takes the form of a chemical signal. The specialized chemicals that carry the signals across the intercellular gaps, or synapses, are called neurotransmitters.
The ebb and flow of neurotransmitters—neurotransmission—is thus an essential feature of the brain's response to experience and the environment. To grasp the basic idea of neurotransmission, compare the brain to a computer. A computer consists of basic units (semiconductors) that are organized into circuits; it processes information by relaying electric current from unit to unit; the amount of current and its route through the circuitry determine the final output. The brain's corresponding basic units are the neurons—100 billion of them; the brain relays information from neuron to neuron using electricity and neurotransmitters; the volume of these signals and their routes through the organ determine what we perceive, think, feel, and do.
Of course, the brain, a living organ, is much more complex and capable than any machine. Brain cells respond with greater versatility to more types of input than any semiconductor; they also can change, grow, and reconfigure their own circuits.

Neuroscientists seeking to understand why a drug is abused and the consequences of that abuse focus on two issues:
Kikosi Kazi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Uwanja wa Ndege wa Dar es Salam (JNIA) jana kilimkamata mwanamke mmoja, Salama Omari Muzara akiwa amemeza kete za dawa za kulevya aina ya Heroin ambazo idadi yake kamili haijajulikana.
Kamishna wa Polisi Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema, msichana huyo alikamatwa jana saa saba mchana akiwa njiani kuelekea Macao, China na Shirika la Ndege la Ethiopia.
“Alikuwa anasafiri kwenda Macao, China kwa ndege ya Ethiopian Airlines ambayo ilikuwa iondoke saa 10 jioni ndipo kikosi kazi cha polisi uwanja wa ndege kikamshuku kuwa amebeba kitu kisicho cha kawaida” alisema Nzowa.
Nzowa alisema, mwanamke huyo alikuwa na hati ya kusafiria namba AB548242 ambayo ilitolewa Oktoba mwaka jana na haikufahamika idadi kamili ya pipi alizomeza kwani mpaka sasa bado anazitoa. Nzowa alisema mpaka sasa mwanamke huyo tayari ameshatoa pipi kadhaa tangu alipokamatwa jana mchana ambapo kuanzia asubuhi leo hadi saa saba mchana huu ameshatoa pipi 27.
Kamishna Nzowa alisema hiyo ni sehemu tu ya mapambano ya dawa za kulevya nchini ambayo imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa wasafirishaji na watumiaji wa dawa hizo.
Hivi karibuni, Mwanamitindo wa Tanzania, Jackline Cliff alikamatwa na kete 66 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya dola za Marekani 137,720 huko Macao, China.
Mwanamitindo huyo , aliyekuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Kamanda Nzowa alisema kikosi chake kinaendelea kuwasiliana na Polisi wa Macao ili kujua iwapo ataweza kurejeshwa nchini ingawa alikiri suala hilo limekuwa gumu kwani China hawana utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
Older Posts Home

Habari za Ulimwengu (audio)

Matangazo ya Radio

Matangazo ya Radio
Aloyce Nyanda

Kutoka Bungeni

Waliokwisha Peruzi

swahilizonetz

swahilizonetz

Habari kwa Kina

Habari kwa Kina

Habari

Afrika afrika mashariki Amani na Ulinzi Asia Makala michezo Siasa Tanzania Uchumi na Biashara Ushirikiano Kimataifa
swahilizonetz. Haki zote zimehifadhiwa.
Imeendelezwa na swahilizonetz