wanafunzi wa chuo huko nigeria
Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe , Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
Afisaa mmoja aliambia BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.
Serikali ya Nigeria ilisema kuwa haitafunga shule zingine kutokana na shambulio lililowaua wanafunzi 50 katika chuo kikuu cha mafunzo ya kilimo
Shambulio hilo linashukiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumapili.Wavamizi walishambulia kwa risasi chuo hicho kilichoko jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Afisa mmoja wa serikali Abdullahi Bego, ameambia BBC kuwa serikali na idara ya jeshi zitaongeza usalama katika taasisi zote za elimu.
Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limewekwa katika hali ya hatari kufuatia mashambulio yanayofanywa kila mara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Boko Haram wanadaiwa kupigana kwa lengo la kuiondoa serikali iliyoko na badala yake kuweka utawala wa kiislamu. Tayari wamefanya mashambulio kadhaa katika shule.
Chanzo BBC
0 Maoni Kuhusu Habari Hii