Timu ya soka ya Real Madrid jana iliwekwa pabaya na mtani wake wa
jadi Atletico Madrid baada ya kunyukwa goli moja kwa nunge katika uwanja
wa Santiago Bernabeu. Kipigo hicho ni cha kwanza cha Atletico Madrid
dhidi ya Rear Madrid tangu mwaka 199.
Kwa ushindi huo, Atletico Madrid imefanikiwa kukusanya pointi zote 21 za mechi saba zilizochezwa tangu La Liga ianze sawa kabisa na bingwa mtetezi Barcelona.
Goli pekee la mchezo huo lilipachikwa kimiani na Diego Costa katika dakika ya 11 ya mchezo huo. Costa sasa anafungana na mchawi wa Barcelona Lionel Messi kwa kila mmoja wao kufunga magoli 8.
Katika mechi iliyochezwa kabla ya hiyo mabingwa watetezi Barcelona walimfunga Almeria mabao mawili kwa nunge. Messi alifunga bao la kwanza kabla ya kujeruhiwa na kupumzishwa na Adriano Correia alifunga la pili.
Real Sociedad imetoka sare ya bao moja kwa moja na Sevilla na Valencia imeichapa Rayo Vallecano bao moja kwa sifuri.

0 Maoni Kuhusu Habari Hii