Kiongozi wa al Qaida akamatwa nchini Libya

Vikosi vya Marekani vimemtia mbaroni kamanda wa ngazi za juu wa kundi la al Qaida nchini Libya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na makomando wa Marekani nchini humo
. Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imesema kuwa, kiongozi huyo wa al Qaida anayeitwa Anas al Liby amekamatwa katika mashambulizi yaliyofanywa jana nchini Libya sambamba na yaliyolenga pwani ya mji wa kusini mwa Somalia dhidi ya wapiganaji wa al Shabab. Hata hivyo wanamaji wa Marekani hawakufanikiwa katika shambulizi la Somalia. Al Liby amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na Marekani kwa madai ya kuhusika katika milipuko dhidi ya balozi za Marekani Afrika Mashariki mwaka 1998.
 George Little msemaji wa Pentagon ameeleza kwamba, Abu Anas al Liby hivi sasa anashikiliwa katika kituo cha kijeshi cha Marekani nje ya Libya. Mashambulizi ya askari wa Marekani dhidi ya Somalia na Libya yamefanyika ikiwa ni wiki mbili tangu jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi lishambuliwe na kundi la al Shabab na kupelekea watu 67 kuuawa.

chanzo radio iran
Vielezo: , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako