MWANZA CITY COUNCIL
MWANZA-TAMPERE
STRENGTHENING COOPERATION PROJECT
Tampere cultural
week 29th October 2013.
Mstahiki
Meya wa jiji la Mwanza,
Kaimu
Mkurugenzi wa jiji la mwanza
Wajumbe
wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi,
Walimu
wa shule za mradi ,
Mabibi
na mabwana.
Wanafunzi
wote kwa ujumla
Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu kwa
wageni wote waalikwa na kwa marafiki zetu kutoka Tampere Finland. Ndugu mgeni
rasmi:
Mradi
wa Uhusiano wa jiji la Mwanza na Tampere ni moja ya Miradi ya Halmashauri ya jiji
la Mwanza hivyo ni Mradi ambao uko chini yako moja kwa moja.
Historia
ya uhusiano na ndugu zetu wa Tampere una takribani miaka 22 hivi sasa, ilikuwa
ni matembezi ya kawaida tu mwaka 1987 ambapo timu ya jiji la Tampere ilipokuja
kutembelea hapa Mwanza wakati huo tukiwa manispaa,matembezi hayo yalipelekeea
kusainiwa kwa mikataba mbalimbali,ambapo mkataba wenye mafanikio zaidi
ulisainiwa mwaka 2000.
Mkataba
huo uliopelekea kuanzishwa kwa mradi utaokaokuwa ukisimamia na kutekeleza
shughuli mbalimbali tunakazokuwa tumekubaliana na wenzetu wa jiji la
Tampere,hivyo ni dhahiri kuwa shughuli zilizotekelezwa na zitakazo tekelezwa na Mradi
huu ni matunda ya ushirikiano kati ya
jiji la Mwanza na jiji la Tampere la nchini Finland.
Baadhi
ya shughuli amabazo zimeshatekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa ni kujengea uwezo mkubwa kikosi chetu cha
zimamoto kwa kukipatia mafunzo ndani na nje ya nchi pamoja na vifaa kama
vitendea kazi ,tumeweza kuotesha miti mingi sana na kuisambaza sehemu
mbalimbali ya jiji letu na tumeweza kutoa mafunzo kwa waheshimiwa madiwani na
watumishi wa halmashauri ya jiji letu,haya ni baadhi tu ya matunda tuliyoweza
kuayapata kupitia uhusiano na wenzetu wa jiji la Tampere.
Ndugu
wageni waalikwa na wadau wote wa mradi na wananchi wa mwanza kwa ujumla, Leo
tunasherehekea Wiki ya Tampere jijini mwanza na wenzetu huwa wanasherehekea
Wiki ya mwanza jijini Tampere Finland.
Mstahiki
meya: Mradi wa Mwanza-Tampere, umejipanga kutoka mafunzo mengi sana katika
idara nyingi kama vile Madiwani wa kata, watendaji na wenyeviti wa Mtaa,
mafunzo ya mazingira kwa ma Afisa afya, walimu na mafunzo ya ushauri na nasaha
kwa walimu wa shule.
Mstahiki
meya, kupitia ushurikiano huu ndani ya miaka kumi tumepata misaada mingi kama
vile gari la kuzimia moto mawili na pia mradi umetoa mafunzo ya compyuta kwa
walimu wafanyakazi wa halmashauri wengi na pia mafundisho haya ni ya kuendelea
kwa muda wote. mradi wa mahusiano ya jiji la Mwanza na
Tampere umepanga kuwapatia mafunzo juu ya demokrasia na utawala bora,ni dhahiri
kuwa mafunzo haya ni ya muhimu sana kwenu katika kuboresha utendaji kazi wenu
katika kata na Halmashauri mnazoziongoza.
Ni vyema kutoa shukrani kwa wasimamizi wa mradi huu kwa kuandaa mipango
mizuri na edelevu kwa kukuza uwezo wa halmashauri yetu katika kuboresha uwezo
wa halmashauri yetu ya Mwanza ili kuweza kuwahudumia wakazi wa mwanza kwa
ujumla . .
Ndugu
mstahiki meya ,Ni matumaini yangu kuwa mtakuwa wasikivu na kuyafuatilia kwa makini mafanikio ya mradi huu
kwa wadau wote ambao tulikuwa pamoja nao kwenye shughuli za mradi.
Ahsanteni
kwa kunisikiliza.
chanzo:halmashauri ya jiji la mwanza.
chanzo:halmashauri ya jiji la mwanza.

0 Maoni Kuhusu Habari Hii