Wachezaji
wa zamani nyota wa Brezilia, ikiwa ni pamoja na mfalme wa kabumbu Pelé,
mrithi wake Zico “Pele blanc” au Luiz Felpe Scolari, meneja wa klabu ya
Seleçao iliyotwaa kombe la dunia katika michuano ya kombe la dunia ya
mwaka 2002, wametoa salaamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji
wa zamani nyota wa Ureno, Eusebio da Silva Ferreira, akijulikana kwa
jina la “chui mweusi”, aliefariki jana asubuhi akiwa na umri wa miaka
71.

Mchezaji nyota wa zamani wa Ureno katika miaka 1966, Eusebio da Silva Ferreira
“Tulitokea kua marafiki ndugu katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1966 nchini Uingereza”, amesema Pelé, akiweka picha waliyopigwa wakiwa wawili katika michuano hio iliyochezwa nchini uingereza.
Katika mchuano huo wa kuwania mshindi katika kundi lilozishirikisha timu hizo, Ureno iliifunga Brezil mabao 3-1, ambapo mabao mawili ya liingizwa wavuni na Eusebio da Silva Ferreira.
Timu hio ilimaliza michuano hio ikijikuta ilichukua nafasi ya tatu.
Zico, mchezaji mwengine nyota wa Brazil,ambae alikua akivalia jezi nambari 10 mgongoni, ametoa pia salaamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji huyo nyota wa zamani wa Ureno, Eusebio.
“Niliwahi kupata fursa ya kucheza nae dakika chache katika warsha ya miaka 50 ya (mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujeremani Franz Beckenbauer), amesema Zico, akibaini kwamba anaifikiria familia ya marehemu, huku akiomba Mwenyezimungu apokeye mikononi mwake.
Meneja wa Brezil, Luiz Felipe Scolari anakumbuka jinsi walivyoanza na marehemu mawasiliano yao kupitia tovuti iitwayo Globo Sports, wakati alikua akiinoa klabu ya Portugal katiaka miaka ta 2003 hadi 2008.
Muilli wa Eusebio umewekwa tangu jana jumapili kwenye uwanja wa Luz mjini Lisbonne, ambako ni makao makuu ya klabu yake ya zamani Benfika.
Mchezaji huyo nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, atazikwa leo jumatatu katika makaburi ya Lumiar, mjini Lisbonne.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii