Hizi mbinu za wauzaji haramu wa dawa za kulevya zinazidi kuibuliwa kila uchao.
Huko Pittsburgh katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani, askari kanzu mmoja amesema alifanikiwa kununua dawa za kulevya aina ya heroin katika moja ya maduka makubwa ya chakula ya McDonald baada ya kupewa taarifa za siri na mtu mmoja.
Mtu huyo alimfahamisha askari kuwa endapo atatumia njia ya kuagiza chakula dirishani huku ukiwa ndani ya gari (drive-thru)

ukisema, “I’d like to order a toy” yaani, “naagiza mwanasesere” basi mfanyakazi atakupa dawa hiyo ya heroin.
Baada ya kutoa oda hiyo, ataelekezwa kwenda kwenye dirisha la kupokelea kama ilivyo kawaida na kila kitu kitakuwa ndani ya boksi lenye chakula na dawa.
Polisi aliyejaribu mbinu hiyo alifanikiwa kupata pakiti 10 za dawa hizo na ndipo alipomtia mbaroni Shantia Dennis, 26, na walipompekua walifanikiwa kumkuta na pakiti 50 nyingine za heroin.
Mfanyakazi mwingine wa McDonald alikamatwa katika mkahawa uliopo Murrysville naye akiuza heroin.
Hii ni hatari kwani sehemu zinazotumika kufanyia mauzo ya dawa hizi ni mahali ambapo si rahisi mtu kuanza hata kuwaza na kuhisi kuwa inawezekana kufanya hivyo.

0 Maoni Kuhusu Habari Hii