Dar es Salaam. Washindi wa pili wa Kombe la Taifa la netiboli timu ya Morogoro imewalalamikia waandaaji Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) kwa kuwanyima kikombe na kuwapa pakiti tatu za majani ya chai kama zawadi
. Kocha wa timu hiyo, Edson Chitanda aliliambia gazeti hili jana kuwa awali Chaneta iliwapa kikombe hicho na kupiga nacho picha kabla ya kuwanyang’anya saa chache baadaye kwa madai kuwa walikiazima hivyo kinarudishwa kilikotoka. “Hatujui hata kiongozi wetu wa Morogoro tutamwambia nini, kwani atakuja kutupokea akijua tuna kikombe wakati Chaneta walitunyang’anya saa chache baada ya kutukabidhi na kutuambia kikombe hicho walikiazima na kinapaswa kurejeshwa kilikotoka,” “Sasa ushindi ndiyo unakuwa hivyo, tukifika Morogoro tunawambia wananchi kuwa tumekuwa wa pili, lakini hatuna kikombe watatuamini kweli? Alihoji kocha Chitanda na kuongeza kuwa walichoambulia kama zawadi kwenye mashindano ni pakiti tatu za majani ya Chai Tausi huku wachezaji wake wakipoteza morali kama timu iliyoingia fainali. Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Kibira alisema, Morogoro wanatakiwa kurudisha kombe la mshindi wa tatu walilotwaa kwenye mashindano yaliyopita kabla ya kupewa hichi ya ushindi wa pili. “Morogoro hawajarudisha kombe la mshindi wa tatu, wanatakiwa kurudisha kwanza hilo kombe ndiyo watapewa la mshindi wa pili waliloshinda Jumamosi,” alisema Kibira. Licha ya kuwa wa pili kwenye matokeo ya Jumla, wachezaji wa Morogoro, Beltina Kazinja aliibuka mchezaji bora wa kati (C) wakati Nasrat Fikiri akiibuka mzuiaji bora (GD) na Andresa Andrew (GA) akiibuka mchezaji bora wa jumla kwenye mashindano hayo yaliyomalizika Jumamosi iliyopita Dar es Salaam kwa Temeke kutwaa ubingwa.

0 Maoni Kuhusu Habari Hii