![]() |
MWENYE KITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WA KUPIGA VITA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA NA UHALIFU TANZANIA {OJADACT) Ndugu Edwini Soko |
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko, Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania, kina mpango wa kupeleka waandishi wake Nchini China ili kujionea sakata la watanzania wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Soko, hali ni mbaya kwa watanzania, kwani wengi wanashikiliwa kwenye magereza Chini China kwa kukutwa na dawa za kulevya, kimsingi amesema kuwa hakuna mawasiliano ya karibu ya kujua idadi ya watanzania walioshikiliwa Nchini humo.
Soko amesema kuwa pia kuna malalamiko toka kwa baadhi ya watanzania wanaoishi Nchini China kunyanyaswa kwa kuhisiwa kuwa ni watu hatari wa madawa ya kulevya.
ODAJACT kimeanza mazungumzo na ubalozi wa Tanzania Nchini China kupitia kwa mmoja wa maafisa wake Bwana Edmund Kitokezi juu ya kuanza mipango ya kuwapeleka waandishi wa habari Nchini humo kujionea hali halisi ili waweze kuandaa ripoti maalumu ambayo itaeleza ukweli juu ya watanzania wanaoshikiliwa nchini humo kwa tuhuma za dawa za kulevya.
Kwa sasa OJADACT zote zilizoelekekwa na ubalozi ili kufanikisha safari hiyo.
Wito. Dawa za kulevya ni hatari kwa jamii,
0 Maoni Kuhusu Habari Hii