CHOCHOEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA

WANAWAKE DAY


KAULI MBIU YA MWAKA 2014




CHOCHOEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA


Afisa Jinsia wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita madawa ya kulevya (OJADACT) Shani Saidi Amanzi amewataka wanawake siku hiyo iwe ni siku pekee ya kuonyesha uelewa wao mjini tu bali waweze kuwakumbuka na wanawake walio vijijini .
Shani amesema wanawake wengi kwa sasa wanaupeo mkubwa wa mambo mbalimbali na wanajitambua mfano mzuri ni bunge la katiba pia usawa wa wanawake na wanaume umetendeka kuwepo bungeni.
Aidha sakata kubwa linalowapa doa wanawake kwa sasa ni matumizi ya madawa ya kulevya ambapo kwa tamaduni za kiafrika tendo hilo ni tendo lenye muonekano kwa mwanamke kuonekana kama mtu mwenye roho ngumu na mwiko kwa mwanamke .
Akiwa kama Afisa Jinsia anayehusika na maswala ya kijinsia hasa watoto na wanawake anasikitishwa sana kuona jamii imebadilika hususani aibu ya mwanamke  haionekani hasa kwenye kufanya maovu  .
Mfano mzuri sakata la kutumika kwa madawa ya kulevya  kwa sasa ni kama  biashara  na matumizi mfano mzuri ni sakata la wanawake wengi maarufu kutumia madawa ya kulevya mfano mzuri ni Masogange na Melisa kukamatwa kule Afrika Kusini na
Jack Patrick ambaye alikamatwa Hongkong china Decemba 19 mwaka 2013 ambaye pia ni mwanamitindo na alikuwa  Miss Ilala Namba 3, 2005, alikamatwa na madawa aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 kwa kuhifadhiwa ndani ya kete 57.

Shani amewataka wanawake na wasichina wanaotumia madawa ya kulevya kutokana na sababu mbalimbali waache kabisa  na kujihusisha na shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo.
Shani amesema kwa kushirikiana na waandishi wa habari atahakikisha mambo ya kijamii hasa kwa watoto na kina mama yanakuwa katika mstari wa mbele katika kuyaandika ,kuyaonyesha na wanajamii kuyasikia  yawe mabaya au mazuri ili kukosoa,kuelimisha  na kukemea ili kuleta maendeleo ndani ya nchi.
Kwani kauli mbiu ya kitaifa  mwaka  huu inasema chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia ambapo kwa mkoa wa Mwanza maandamano yataanza kuanzia Nyakato sokoni paka shule ya msingi Nyakato kata ya Mahina.




Vielezo: , , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako