Jeshi
la Polisi Nchini litaendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia na vitendo vya mauaji yanayosababishwa na Imani za kishirikina
kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IJP Ernest Mangu katika mkutano mkuu wa maofisa wakuu waandamizi unaoendelea katika chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA) ukiwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Weledi katika Kutoa Huduma bora kwa jamii”.

JP
Mangu alisema kuna baadhi ya jamii zinafanya vitendo hivyo kama tamaduni
zao hivyo wao kwa kuliona hilo wataendelea kutoa elimu kwa njia
mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ili kuhakikisha kuwa
vitendo hivyo vinakomeshwa hapa nchini.
“Tuendelee kutoa elimu kwa jamii lakini pia tutaenelea kuchukua hatua kwa wote wanaofanya makosa hayo kwa kuwa huo ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine” Alisema IJP Mangu.
Naye Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amewataka Makamanda wa Polisi wa mikoa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali katika kutatua migogoro ya Ardhi ili kuipatia ufumbuzi mapema kabla ya vurugu kutokea jambo ambalo litaendeleza usalama hapa nchini.
Alisema ni vyema Taasisi husika kushirikiana mapema katika kutatua migogoro katika jamii kabla haijaleta madhara kwa kuwa iwapo hilo litafanyika itaepusha uharibifu na gharama ambazo hutumika katika kutatua mgogoro unapokuwa mkubwa na kusababisha vurugu.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Jamii nchini Mussa Ali Mussa alisema wataendelea kutumia dhana ya Polisi Jamii katika kupambana na uhalifu kabla haujatokea kwa kuwa wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa tangu kuanzishwa kwa dhana hiyo.
Alisema kwa Mujibu wa Utafiti uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ufadhili wa COSTEC umeonyesha kuwa Asilimia 70 ya watanzania wamekubali dhana ya Polisi Jamii na wameonyesha kuikubali kwa kuwa imesaidia kupambana na uhalifu unaotokea katika maeneo yao.
Mkutano huo unaoendelea katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi una lengo la kujadili na kufanya tathmini ya mafanikio yaliyofikiwa mwaka 2013 pamoja na changamoto zilizopo katika kupambana na uhalifu na kuzipatia ufumbuzi kwa mwaka 2014.

0 Maoni Kuhusu Habari Hii