M23: Serikali ya Kongo imekiuka makubaliano

Kundi la waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kukiuka sheria ya msamaha kwa waasi wa kundi hilo.
Taarifa iliyotolewa na Tawi la Kisiasa la kundi la M23 imesisitiza kwamba serikali ya Kongo kabla ya kutangaza msamaha, ilitoa orodha ya majina ya mamia ya wanachama wa kundi hilo akiwemo Jenerali Sultani Makenga na baadhi ya makamanda wengine wa kundi hiyo, na kueleza kwamba watu hao hawana sifa za kupewa msamaha. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua ya kutayarishwa orodha hiyo inakinzana waziwazi na taarifa ya pamoja iliyotolewa Nairobi, Kenya  pamoja na msamaha waliopewa waasi wa kundi hilo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Februari mwaka huu, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alitangaza msamaha kwa waasi wote wa kundi la M23, isipokuwa wale waliotenda jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu.
Vielezo: , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako