Uchunguzi wa kina wa Swahilizone umethibitisha kuwa baadhi ya
wakazi wa mpaka wa Niger na Nigeria wamekuwa wakishirikiana na
wapiganaji wa Boko Haram ili walipwe pesa.
Nchi zilizo jirani na Nigeria, kama Niger,
Cameroon, na Chad zinahofia kuwa harakati za wanamgambo hao zitaathiri
usalama wa nchi hizo.Kulingana na Thomas Fessy ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi huo akiwa eneo la Diffa kusini mashariki mwa Niger katika mpaka na Nigeria, wanachama wa genge hilo ambao wengi wao ni vijana walio na umri wa miaka kati ya 20 na 25 wameiambia BBC kuuwa vikundi vyao vitano vimeshajiunga na Boko Haram; na wawili tayari walishauawa katika operation walizojihusisha nazo.
Lakini wamesisitiza wao hawana haja na kupigania uwepo wa sheria za kiislamu , haja yao ni hizo pesa.
Maafisa wa usalama katika eneo hilo wanasema wamemudu kuzuia mashambulio kadhaa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita na watu kadhaa wanaoaminika kuwa na uhusiano na Boko Haram wamekamatwa.
Ni dhahiri kuwa Boko Haram wanaendeleza vitendo vyao vya kikatili hadi kuvuka mpaka wa Nigeria.
Umoja wa mataifa unasema tayari watu wapatao 50,000 washavuka mpaka kuingia Niger kujaribu.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii