UN kutuma wanajeshi wa kulinda amani CAR

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma kikosi kipya cha wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-kikosi hicho kitawajumuisha wanajeshi karibu alfu kumi na mbili.

Kwa sasa kuna wanajeshi alfu sita wa kikosi cha umoja wa Afrika pamoja na alfu mbili kutoka Ufarnsa, lakini vikosi hivyo vimekabiliwa na wakati mgumu kurejesha utulivu.
Maelfu wamefariki duniani na takriban watu milioni moja wamelazimika kutoroka makwao kufuatia vurugu zilizodumu kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anasema kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na mzozo unaoibua wasiwasi-- ambapo wanamgambo wa mirengo pinzani ya kidini wanaendelea kupigana huku msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza ukitishia zoezi la kusambaza misaada kwa waathiriwa.
Zaidi ya raia thelathini waliuwawa katika mapigano ya hivi punde katika mji wa Dekoa katikati mwa taifa hilo.

Chanzo:BBC
Vielezo: , , , , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako