
Wapinzani wa raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza wamepuuza agizo la serikali la kuwataka wasitishe maandamano ya wiki mbili wakilitaja agizo hilo kuwa sawa na kutangaza vita.
Hadi sasa watu 18 wameuawa tangu rais Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula wa tatu kwenye uchaguzi wa mwezi ujao.
Habari zinazotufikia zinasema kuwa watu wawili zaidi wamedaiwa kuuawa katika maandamano hayo na kuongeza idadi ya waliouwa kufikia 20.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii