Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon anazuru
eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo ambako kumekuwa na
mapigano ya siku tatu kati ya vikosi vya serikali na waasi wa m23.
Ban anatarajiwa kukutana na wanachama wa kikosi
kipya cha umoja wa Mataifa ambacho kimeundwa ili kukabiliana na makundi
ya waasi katika eneo la Maziwa Makuu.Ziara hiyo inakuja siku moja
Eneo la Mashariki mwa DRC, nlimenaswa katika miaka ishirini ya vita kati ya wanajeshi wa makundi ya waasi wanaaminiwa kuungwa mkono na Rwanda pamoja na waliokuwa washirika wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Kuna matarajio mengi kuwa kikosi hicho cha UN kitaleta utulivu katika eneo hilo lenmye utajiri mkubwa wa madini.
Mapigano yanaendelea kati ya majeshi ya serikali na waasi wa M23 katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mapigano hayo yanatokea wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na mkuu wa benki ya Dunia Jim Yong Kim wakizuru taifa hilo.
Mashambulio yamezidi katika makaazi ya raia.
Wapiganaji hao wa M23 walikuwa wameahidi kusitisha mapigano wakati wa ziara hiyo ya Ban Ki Moon
chanzo bbc
0 Maoni Kuhusu Habari Hii