Mbowe: Serikali inawafahamu wahusika wa bomu

 
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa, vinawafahamu watu waliohusika na mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho. Mbowe, amesema tukio hilo ni la kisiasa na lilipopangwa awali. Amesema wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kuhatarisha demokrasia ya vyama vingi nchini tanzania. Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na makamishna wawili, kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo. Mbowe amesema ni bora serikali itangaze kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala. Amesisitiza kuwa, uchunguzi wa awali katika eneo la tukio umebaini kuwa bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa kwa mikono
Vielezo: , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako