Rais wa Togo azikosoa vikali nchi za Magharibi!


                                                            Rais Faure Gnassingbé wa Togo
Rais Faure Gnassingbé wa Togo amezikosoa vikali nchi za Magharibi kwa kukata misaada yao kwa nchi hiyo na kusisitiza kwamba hatua hiyo itazidisha  vitendo vya kigaidi nchini humo.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kinachojadili maswala ya  ugaidi barani Afrika, Rais Gnassingbé  ameongeza kuwa, nchi za Magharibi zilichukua hatua za kidhulma kwa kukata misaada yao kwa serikali ya Lome mwaka 2008. Rais Faure Gnassingbé Ameongeza kuwa, nchi za Magharibi zinapasa kutekeleza ahadi zao ilizozitoa kwa nchi zinazoendelea na hasa za Kiafrika, ili uchumi wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika ukue na kufikia kiwango cha asilimia 7 mwaka 2015.
Vielezo: , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako