Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na
mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini
Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndungu Githinji amesema kuwa wana habari kuwa kambi zilizoko kwenye mipaka ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kiislamu.
Kenya inahifadhi wakimbizi wa kisomali zaidi ya nusu milioni katika kambi za Dadaab zilizoko kwenye mpaka na Somalia.
Mwenyekiti huyo Ndungu Githinji ameambia SWAHILIZONE kuwa miaka 22 imetosha kwa usaidizi kwa wasomali hao na wanastahili sasa kurudi nyumbani baada ya amani kurejeshwa nchini mwao.
''Hawa wakimbizi wamekaa miaka ishirini na mbili Kenya. Ningependa kuuiomba UN ifunge kambi hizo. Iwarudishe wasomali kwao, maana sasa nao pia wanayo serikali yao. Ili tuweze kukaa kwa amani.''Amesema bwana Githinji.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii