Venezuela yamfukuza balozi wa Marekani

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametangaza  hatua ya kuwafukuza mabalozi wa Marekani nchini, ikiwa pamoja na mwakilishi mkuu Kelly Keiderling. Wengine ni watumishi wawili wa ubalozini.
Wanadiplomasia hao wamepewa muda wa saa 48 kuondoka nchini Venezuela. Rais wa Venezuela amesema kuwa anao ushahidi wa shughuli za kuvunja sheria za mabalozi hao. Hata hivyo Rais Maduro hakutoa maelezo zaidi juu  ya shughuli za Wamarekani hao licha  ya  kufahamisha kuwa walikutana na viongozi wa  upinzani na wa vyama vya wafanyakazi katika jimbo  la kusini magharibi mwa Venezuela.    
Vielezo: , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako