Myanmar yakataa kuwapa Waislamu uraia

Serikali ya Myanmar imekaidi azimio la Umoja wa Mataifa ambalo liliitaka iwape uraia Waislamu wa kabila la Rohingya waliowachache na wanaodhulumiwa nchini humo.


Jumanne wiki hii kamati ya haki za binaadamu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio ambalo pia liliitaka serikali ya Wabuddha waliowengi Myanmar kuzuia mateso na hujuma dhidi ya Waislamu nchini humo. Msemaji wa serikali ya Myanmar Ye Htut amedai kuwa Waislamu hawana haki ya kupewa uraia.
Kuanzia mwezi Juni mwaka jana magaidi wa Kibuddha wamekuwa wakiwashambulia Waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine ambapo hadi sasa maelfu ya Waislamu wameuawa huku wengine karibu laki mbili wakiachwa bila makao. Aidha Mabuddha hao wenye misimamo mikali wameteketeza misikiti na vijiji vya Waislamu na kupelekea wengi wakimbilie katika nchi jirani ya Malaysia ambayo wakaazi wake wengi ni Waislamu.
Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yanasema Waislamu wanauawa kwa umati huko Myanmar huku dunia ikinyamazia kimya ukatili huo.
Vielezo:

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako