Sudan yasema waasi wanajaribu kuharibu nchi

Mkuu wa idara ya usalama na upepelezi nchini Sudan, ameyatuhumu makundi ya waasi kuwa yanafanya njama za kudhoofisha na kuharibu usalama wa nchi hiyo na nchi nyingine za eneo. Muhammad Atau Maula Abbasi ameyasema hayo leo katika kikao cha kamisheni ya vyombo vya usalama na intelijensia vya Afrika (CISSA) kilichofanyika mjini
Khartoum na kuongeza kuwa,  kundi la waasi la “Uadilifu na Usawa” lenye kuendesha harakati zake katika jimbo la
Darfur nchini humo, ndilo lililohusika katika tukio la kumteka nyara Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan. Itakumbukwa kuwa Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan, alitekwa nyara mwezi uliopita na kisha akaachiwa huru baada ya masaa kadhaa. Aidha Abbasi ameongeza kuwa, baadhi ya nchi za Kiafrika zimekuwa zikiyaunga mkono makundi ya waasi ambayo yanakabiliwa na hali mbaya ya kusambaratika kwa lengo la kuchafua usalama wa nchi nyenginezo katika eneo. Amesema kuwa mbali na makundi hayo ya waasi kutekeleza mashambulizi katika kuwalenga wanajeshi na ofisi za serikali, lakini pia wanawashambulia wananchi na kuwaua bila hatia.
Vielezo: , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako