Walcott kurudi uwanjani?

Theo Walcott huenda akaichezea Arsenal siku ya jumaamosi ikiwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili baada ya kupona kutokana na majeruhi ya tumbo.


Walcott yumo katika kikosi cha kupambana na klabu yake ya zamani Southampton siku ya Jumaamosi.

"hajachezea hata kikosi cha akiba lakini nitamjumuisha katika kikos ikamili cha Jumaamosi '' alisema kocha Arsene Wenger.Walcott mwenye umri wa miaka 24-aliumia katika pambano la ligi dhidi ya Stoke September 22 baada ya kutegua maumivu aliyopata katika pambano la siku nne zilizotangulia dhidi ya Marseille.
"yuko mzima kabisa."
Awali Wenger alimtumia Serge Gnabry kuchezea nafasi iliyoachwa na Walcott, lakini tangu wakati huo safu yake ya kiungo ilimaarishwa na kurejea kwa Mikel Arteta naJack Wilshere.
"Theo ana sifa tofauti na wachezaji wengine na nimefurahi sana kwamba amerejea" alisema Wenger
chanzo bbc
Vielezo:

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako