. Akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya mabatini line polisi, katika hotuba yake kamanda Mangu alivipongeza na kuvishukuru vikundi hivyo vya kijinsia na kusema kuwa kazi hizo za kuzuia unyanyasaji na ukatili wa kijinsia mara ya kwanza shughuli hizo zilifanywa na jeshi la polisi pekee.
Katika kupambana na unyanyasaji wa kijinsia jeshi la polisi limeaanzisha Dawati maalumu kwa kushirikiana na vikundi shirikishi vya kupambana na ukatili wa kijinsia . Dawati linafanya kazi yake vizuri na kwa ufanisi mkubwa kuhakikisha linaweza kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
Alisema jeshi la polisi mpaka sasa limeshikilia na kuwafikisha mahakamani watu 134 katika mkoa mwanza akitoa takwimu hizo amezitaja wilaya zinazoongoza kwa ukatili pamoja na mauaji ya vikongwe.wilaya za kwimba misungwi na magu.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa mkoa wa mwanza wakiwemo madiwani,viongozi wa kidini watendaji wa kata, wenyeviti serkali za mitaa na viongozi kutoka taasisi mbali mbali za kijinsia.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa taasisi ya KIVULINI Ndugu Ramadhani Masele alisema taasisi yake inajitaidi sana kumbana na unyanyasaji mkubwa kwa kuzipeleka kesi mahakamani lakini wanakutana sana na vikwazo kutoka katika familia haswa kesi zinapokuwa katika hatua ya hukumu .
Maandamano hayo yalifanyika siku ya jumatatu yakianzia katika bustani za Mahatma Ghandhi na kupitia barabara za uhuru na nyerere Road
0 Maoni Kuhusu Habari Hii