Habari na Mwandishi wetu.Simba Kabonga-Mwanza
Viongozi wa chama cha soka cha wilaya ya ilemela(IDFA) Wamekabidhiwa zawadi kwa ajili ya washindi na wanamichezo bora wa ligi yao daraja la Nne iliyomalizika hivi karibuni
Akiongea na vyombo vya habari wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa kampuni ya barmedas.com, Kampuni amabayo inadhamini ligi za ilemela na nyamagana Mr Hirnoy Barmeda alisema kampuni yake imedhamini ligi hizo kwa mkataba wa miaka mitano alisema anafuraha kubwa kuona ligi ya idfa imekuwa miongoni mwa ligi bora na yenye ushindani mkubwa nchini Tanzania hasa jijini mwanza
Alisema kwamba kampuni yake inajitolea kudhamini ligi hizo kwa miaka yote hii mitatu ya mkataba bila kuwa na washirika na wadau mbali mbali hivyo aliwaomba makampuni mbalimbali ya kibiashara,watu binafsi kushirikana nae ili kuzidi kuendelea kutia chachu katika ligi hiyo.
Aliitoa zawadi hizo kwa kipa bora,Mfungaji bora,Mchezaji bora,na Mwamuzi bora wa ligi pia kwa team shiriki ambazo ni mabingwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki nne.
Akipokea zawadi hizo katibu mkuu wa idfa Juma Msaka alishukuru kampuni ya barmedas .com kwa ufadhili wa hali na mali kwa chama cha idfa. Alisema kuwa udhamini wao umeongeza hamasa kubwa katika ligi hiyo
na kuahidi kuwa kwa upande wao watatoa mchangao wao kutafuta makampuni na wadau mbali mbali wa michezo kusaidiana na kampuni hiyo katika udhamini. Peter Mumbala wa polisi mwanza aliibuka mfungaji bora wa ligi hiyo
Michezo yote ya ligi za wilaya ya ilemela na nyamagana zinaoneshwa Live na kituo cha barmedas television kupitia channel yake ya michezo ambacho ni barmedas.tv 24/7sports kutoka viwanja mbali mbali vya jiji la mwanza na manispaa ya ilemela...

0 Maoni Kuhusu Habari Hii