Baridi kali yashuhudiwa Marekani

Msimu wenye maridi kali kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani katika miongo miwli iliyopita, unaelekea kupiga maeneo ya Kusini na Mashariki mwa nchi hiyo.
Miji ya New York na Washington ni miongoni mwa miji ambayo imekumbwa na theluji pamoja na baridi kali inayokuja kwa upepo mkali kutoka katika bahari ya Arctic.
Huku baridi ikizidi, gavana wa New York (Andrew Cuomo) amesema kuwa huenda baadhi ya barabara kuu zikafungwa.
Hali hii mbaya ya hewa imelazimisha kufungwa kwa shule huku biashara nyingi zikitatizika hata na safari za ndege pia zimekatizwa pakubwa.
Mamilioni ya watu wameonywa wasitoke nje.
Eneo lenye baridi kali ni Babbitt na Minessota. Theluji hiyo imesababishwa na hewa yenye baridi kali inayotoka katika bahari ya Arctic.

chanzo bbc
Vielezo: , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako