Polisi nchini Iraq wamesema mashambulizi matatu ya mabomu yaliyotokea
mjini Baghdad yamesababisha vifo vya watu 11 na wengine 45 kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari na kando ya
barabara yalitokea katika masoko mawili na mtaa wenye maduka ulio
katikati ya Baghdad. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana watu 8,868
waliuawa katika mashambulizi ya kigaidi na mapambano ya kimabavu
yaliyotokea katika sehemu mbalimbali nchini Iraq.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii