Utumiaji wa madawa ya kulevya ni mojawapo ya mabalaa makubwa yanayoathiri binaadamu na ulimwengu kijumla. Watu wengi wameathiriwa na janga hili biladi/miji zetu
. Kwa
mfano, ndani ya viunga vya jiji la Mombasa pekee inasadikika kuna zaidi
ya vituo/vijiwe arubaini vya usambazaji na utumiaji wa madawa ya
kulevya: http://en.wikipedia.org/wiki/Recreational_drug_use_in_Kenya.
Na kwa upande wa Zanzibar karibu asilimia kumi ya wakaazi wake
wameathirika na madawa hayo. (The Guardian 1/02/2011). La kuhatarisha na
baya zaidi ni kuwa wengi wanaotumia madawa haya ni wanaume baina ya
umri wa miaka ishirini hadi thalathini na tano ambao ndio uti wa mgongo
wa nguvukazi ya umma.
SABABU ZA KUENEA MADAWA YA KULEVYA KATIKA JAMII.
Moja
kati ya udhaifu mkubwa wa mfumo wa kidemokrasia/kibepari ni kule kumpa
mwanaadamu aina nne za uhuru. Kuanzia uhuru wa itikadi, kujieleza,
kumiliki na ‘uhuru binafsi’. Kwa kisingizio cha ‘uhuru wa binafsi’
mwanaadamu hupewa mamlaka ya kufanya alitakalo namna atakavyo, ilimradi
nafsi yake inapenda kufanya hivyo. Hivyo basi, lau mwanaadamu ataamua
kulewa, kuvuta bangi, kuzini, kuvuta kokeni nk. huwa ni sawa. Hii ni
moja ya sababu kuu ya msingi inayopelekea kuongezeka sana vitendo vya
uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya
Aidha,
kuwepo serikali tegemezi katika nchi zetu changa hususan serikali za
ulimwengu wa tatu yaani serikali maskini za kimada/kimali na
zinazoburuzwa kifikra hupelekea serikali hizi kunyenyekea kwa
warasilimali/mabepari ili kupatiwa mikopo ambayo ina masharti magumu.
Ikiwemo kuruhusu au kuanzisha kampuni za ulevi. Kwa mfano, kampuni ya
ulevi ya Malta Tanzania nk . Hii maana yake hata kama ulevi huu sio wa
madawa ya kulevya lakini ni ulevi. Na kwa hivyo hakuna sababu
itakayomzuia mlevi wa kinywaji cha majimaji kutumia madawa ya kulevya
akitaka kutumia kwa kuwa vyote ni vilevi. Na kimsingi kuwepo aina hii ya
vilevi vya majimaji ndiko kunakokuza utamaduni ndani ya jamii kwa umma
kuzoea ulevi kama kitu cha kawaida.
Ukosefu
wa ajira kwa vijana: Kiwango cha ukosefu wa ajira kipo juu sana kiasi
cha kusababisha vijana wengi kukaa ovyo bila ya chochote cha kufanya na
si ajabu kugeukia madawa ya kulevya. Hii inatokana na ukweli kwamba
Mfumo wa kidemokrasia/kibepari hudumaza mazingira ya kiuchumi kwa
kunufaisha matajiri tu na sio jamii kwa ujumla wake. Na hilo hupelekea
kudumaza fikra na viwiliwili vya vijana na maisha ya kuchanganyikiwa, hali ambayo baadhi yao huona ufumbuzi wake ni kutumia madawa ya kulevya.
Vijana
kuishi, kukaa na kuamiliana marafiki waovu katika jamii ikiwemo
maskuli, mabarazani, mahala pa kazi nk. Wengi wanaotumia madawa ya
kulevya katika ukanda wanakubali kwa kukiri kwamba walianza kufanya
hivyo kwa sababu tu marafiki
zao walikuwa wanatumia. Suala hili nalo kwa upana wake hurejelea katika
mfumo wa jamii kwa ujumla, kwa kuwa mfumo unaosimamia jamii ni mbovu
kimaumbile huzalisha wanajamii waovu, pia hutarajiwa sana wengi wa
marafiki ambao kijana hunasibiana nao mara kwa mara katika mazingira
yake nao watakuwa waovu.
Bila
ya kusahau fikra na mawazo potofu waliyonayo baadhi ya vijana wengi
wanaotumia madawa haya. Wao hudai ati madawa hayo yanawapatia ujasiri wa
kuzungumza, kutenda mambo mbali mbali ikiwemo pia huwaondoshea mawazo
machafu na kuwajenga hali ya kujiamini. Kama vile baadhi wanavyodai kuwa
bia inaongezea damu na kuchangamsha siha ya kiwiliwili cha mwanadamu.
ATHARI YA MAADAWA YA KULEVYA KATIKA JAMII
Kukithiri
kwa wizi. Kwa kuwa madawa haya ni uraibu unaopelekea vijana kuwa vigumu
kukaa bila ya kutumia. Na kwa kuwa madawa haya ni ghali, na la
kusikitisha ni kuwa vijana watumiaji wa madawa haya hawana ajira. Hii
inamaanisha kwamba watajihusisha na mbinu wanazozijua zikiwemo za haramu
ili waweze kupata uraibu huo. Na hapana shaka wengi wao hujishirikisha
katika vitendo vya wizi ambavyo huhatarisha usalama wao na jamii
kijumla. Hali hiyo husababisha pia uadui baina ya watu katika jamii.
Bila ya kusahau kupotea heshima ya watumiaji madawa na kuwavunjia watu
heshima zao kama kuwatukana, kuwaudhi nk. Kubwa zaidi janga hili
humsahaulisha mja kumkumbuka au kumtaja Mola wake na kusali. Amesema Allah Taala:
إِنَّمَايُرِيدُالشَّيْطَانُأَنْيُوقِعَبَيْنَكُمْالْعَدَاوَةَوَالْبَغْضَاءَفِيالْخَمْرِوَالْمَيْسِرِوَيَصُدَّكُمْعَنْذِكْرِاللَّهِوَعَنْالصَّلاَةِفَهَلْأَنْتُمْمُنتَهُونَ (المائدة: 91)
Hakika
shetani anataka kukutilieni uadui na bughudha baina yenu kutokana na
ulevi na kamari na anataka kukuzuieni kumkumbuka M/Mungu na[ kukuzuieni]
kusali.Basi je, mtaacha[ mabaya hayo]? (TMQ 5: 91)
Kuenea
kwa maradhi. Leo kuna maradhi mengi ambayo vijana wanaotumia madawa ya
kulevya wanayapata. Baadhi yao humalizikia kuwa wendawazimu kamwe! Maradhi
haya yanawapata vijana hawa kwa kiasi kikubwa na hupelekea jamii
kupoteza rasilmali kubwa ya nguvu kazi. Pia watumiaji wa madawa huambukizana baina yao maradhi
ambukizi kwa kubadilishana sindano. Jambo hili imesababisha pia
kusambaa kwa kiasi kikubwa kwa maradhi ya ukimwi na maradhi mengine
katika miji yetu.
Kifo, mwishowe athari hizi zote ni kuelekea kaburini. Kiwango cha vifo kutokamana na madawa ya kulevya vinaongezeka
kwa kasi mno katika miji ya Waislamu. Vijana wengi hufariki dunia
katika umri mdogo. Vifo hivi vinasababishwa hasa na maradhi yanayoletwa
na madawa ya kulevya. Jambo hili linatia jamii wasiwasi na khofu kubwa
kwa watoto wao, ndugu au jamaa zao wanaotumia madawa haya. Ingawa suala
la kifo ni qadhaa ya Allah Taala, lakini mwanaadamu anatakiwa kuchukuwa
hadhari katika masuala yaliomo katika mamlaka/mzunguuko yake, kama vile
kujikinga na hatari inayomkabili nk. Na lau hakuchukuwa hadhari hiyo
ipasavyo ataulizwa siku ya Kiama kwa nini amejidhulumu.
SULUHISHO
Kitu
cha mwanzo cha lazima kwa Muislamu ni kujifunga na kuufata Uislamu kwa
kumuitikia Allah Taala kwa kufuata amri zake na kuacha makatazo yake
ikiwemo kujiepusha na kila aina ya ulevi. Allah Taala anasema:
يَاأَيُّهَاالَّذِينَآمَنُواإِنَّمَاالْخَمْرُوَالْمَيْسِرُوَالأَنصَابُوَالأَزْلاَمُرِجْسٌمِنْعَمَلِالشَّيْطَانِفَاجْتَنِبُوهُلَعَلَّكُمْتُفْلِحُونَ (المائدة: 90
“Enyi
mlioamini!Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa [kuomba] asiyekuwa
M/Mungu,na kupiga ramli,[yote haya] ni uchafu [ni] katika kazi za
shetani.Basi jiepusheni navyo,ili mpate kufaulu[kutengenekewa]”.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ 24
“Enyi waumini muitikieni M/Mungu na Mtume wake wanapokuiteni katika yale yenye kuleta uhai.”
إِنَّمَاكَانَقَوْلَالْمُؤْمِنِينَإِذَادُعُواإِلَىاللَّهِوَرَسُولِهِلِيَحْكُمَبَيْنَهُمْأَنْيَقُولُواسَمِعْنَاوَأَطَعْنَاوَأُوْلَئِكَهُمْالْمُفْلِحُونَ (النور: 51
“Haiwi
kauli ya waumini wanapoitwa kwa M/Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina
yao,ila husema :”Tunasikia na tunakubali”,na hao ndio watakaofuzo”.
Na
kubwa zaidi ni wajibu Waislamu kukemea uovu huu kwa kufanya bidii
kuzuia kifikra na kubeba mas’ulia/majukumu yetu ya malezi ipasavyo. Huku
tukishiriki kikamilifu katika wajibu wa kubadilisha mfumo ulipo wa
kidemokrasia/ kibepari unaozalisha uovu huu kwa kurejesha
tena maisha ya Kiislamu kwa kupitia kusimamisha tena serikali ya
kiislamu ya Khilafah rashida ili kuokoa maisha ya vijana na ulimwengu
kwa ujuml
0 Maoni Kuhusu Habari Hii