Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuungana kwa pamoja katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama nchini Ethiopia, Rais uhuru Kenyata
amesema makundi ya kigaidi yamejifunza mbinu mpya za kutekeleza hujuma zao na kwa mantiki hiyo ametaka serikali za nchi mbalimbali kuimarisha uwezo wa vyombo vya usalama ili kukabiliana na changamoto zilizoko kwa sasa duniani. Akizungumzia mgogoro wa Somalia, Rais Kenyatta amesema juhudi zaidi zinapaswa kufanywa kwani ukosefu wa amani katika Pembe ya Afrika unaweza kusambaa nje ya eneo hilo na kuwa tatizo kubwa katika siku za usoni. Rais wa Kenya leo atahutubia mkutano mwingine wa kiusalama nchini Jordan ambao utawakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika katika mji wa Akaba.

Tangu Kenya ipeleke majeshi yake nchini Somalia miaka minne iliyopita, nchi hiyo ya Afrika Mashariki imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na kundi la kigaidi la al-Shabab la Somalia ambalo linadai mashambulizi yake ni ulipizaji kisasi wa kuendelea kuwepo jeshi la Kenya katika nchi yao.
Chanzo idhaa kiwahili tehran
0 Maoni Kuhusu Habari Hii