Waafrika Kusini waandamana kupinga xenophobia

Waafrika Kusini waandamana kupinga xenophobia
Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini wameandamana katika mji mkuu wa kibiashara wa nchi hiyo, Johannesburg
, kupinga mashambuliji yanayowalenga raia wa nchi za kigeni.
Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara za kupinga mashambulizi hayo na kubeba mabango yenye ujumbe: "Sisi Sote ni Waafrika".
Waziri Mkuu wa mkoa wa Gauteng, David Makhura, ambaye amehutubia waandamanaji hao amesema Waafrika Kusini watashinda chuki na mashambulizi yanayowalenga raia wa kigeni kama walivyoshinda utawala wa ubaguzi wa rangi.
Mashambulizi ya wiki kadhaa dhidi ya raia wa kigeni katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kama Johannesburg na Durban, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua saba huku polisi ikishindwa kudhibiti watu wanaoshambulia raia wa kigeni. Mashambulizi ya sasa dhidi ya raia wa kigeni nchini Afika Kusini yanakumbusha yale ya mwaka 2008 ambayo yaliua watu 62 katika vitongoji vya jiji la Johannesburg
Vielezo: ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako