ZITTO AJIBU MAPIGO, ASEMA HATOKI CHADEMA LABDA WANITOE WAO

ZITTO KABWE NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA PICHA MAKTABA YA BUNGE
ALIYEKUWA naibu katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini, Mh. Zitto Kabwe hii leo  kAsema yeye  hatagong'oka na kwamba yeye atakuwa wa mwisho kutoka katika chama hicho tena kwa hiyari yake bila kushurutishwa na mtu
,
Hayo ameyasema mapema hii leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Daresalaam, Zito amesema tuhuma ambazo zimeelekezwa kwake kwa kweli zimemfadhaisha sana na kumsumbua sana kimawazo huku tuhuma hizo zikiwa hazina ukweli wowote juu yake,

Kuhusu Walaka zito ameukana waraka huo kuwa hautambui nakwamba watu walioandaa waraka huo walikuwa na lengo la kuwagombanisha chama hicho kikuu ambacho kwa sasa wakati wa uchugazi unakaribia watu wanaamua kuwachanganya

Zito na Dr Mkumbo kupitia kwa wakili wao, wamemtaka mwanasheria mkuu wa chama cha chadema kuudhilishia ummma kwa namna gani watumiwa wametenda kosa kwa kuleta mbele ushahidi usio wa mashaka ili watuhumiwa nao wajibu kwa siku hizo kumi na nne ambazo wateja wake wamepewa,

Aidha mwanasheria kwa upande wake amesema kwa sasa wateja wake hawana haja ya kujibu hoja yoyote kwani tuhuma ambazo zimetaja kwa wametaja wake haziko kimaandishi na badala yake yamesikika kupita vyombo vya habari

Chama kina utaratibu wake wa kupashana habari, sio kwa kutumia vyombo vya habari ndio iwe taarifa rasmi kwa kwa wanachama wake, aliongeza Bwana Albart ambaye pia ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho

 
Vielezo: , , , ,

Swahili Zone

Tovuti huru habarishi (blogu) inayoendeshwa kiueledi yenye lengo mahususi la kuifikishia jamii habari, makala na matukio wakati muafaka inapowezekana kufanya hivyo!

0 Maoni Kuhusu Habari Hii

Andika Maoni Yako