Mpatanishi mkuu upande wa waasi kwenye mgogoro wa
Sudan Kusini, ametoa wito wa kuwepo suluhu la kisiasa akisema kuwa ndilo
jibu la kipekee kwa mzozo huo.
Mpatanishi huyo (Taban Deng Gai) alitoa matamshi yake katika mazungumzo ya amani yanayoendelea kati ya pande zinazozozana mjini Addis Ababa Ethiopia.
Mwakilishi wa serikali Michel Makuel, alisema kuwa upande wa serikali umejitolea kuhakikisha kuna amani na kuwamba vifo vinavyosababishwa na mapigano sharti vikome.
Makabiliano kati ya upandea serikali ya Rais Salva Kiir na waasi wanaoongozwa na aliyelkuwa makamu wa Rais Riek Macahr, yamesababisha maelfu kutoroka makwao.
Awali, viongozi wa Sudan na Sudan Kusini, ambao wakati mmoja walikuwa mahasimu wakuu wa kisiasa wakati wa vita vya uhuru wa Sudan Kusini, walikutana kujadili , kutumia kikosi cha pamoja kulinda visima na mabomba ya mafuta Sudan Kusini dhidi ya kutekwa au kuharibiwa na waasi wakati vita hivi vinapoendelea.
0 Maoni Kuhusu Habari Hii